Kila siku ya wiki, TUKO.co.ke inakupakulia kwa mukhtasari matukio na habari muhimu zilizogonga vichwa vya habari wiki hii ili ukapate kufahamu kwa upana na utendeti mambo yalivyo ulimwenguni.
Wakazi wa Kisumu Jumanne Juni 1 walimpokea Naibu Rais William Ruto kwa shangwe baada ya sherehe za Madaraka Dei.
Maafisa wa usalama wa Ruto walikuwa na kibarua kikali kukabiliana na wafuasi hao waliokuwa wamechangamka pakubwa.
2. Usalama wa Rais: Jamaa Ajaribu Kumkaribia Uhuru Jukwaani Akihutubia Taifa
Jamaa mmoja mwenye umri wa makamo alinaswa na polisi akielekea jukwaani alipokwa Rais Uhuru Kenyatta akilihutubia taifa wakati wa sherehe za 58 za Madaraka dei.
Mwanamume huyo aliibuka kutoka kwa umati wakati Uhuru akihutubu na kuanza kukimbia uwanjani akitatiza sherehe kwa muda, lakini maafisa wa usalama walichukua hatua ya haraka na kumbeba juu kwa juu.
3. Mganga Akamatwa Baada ya Kumtepeli Meneja wa Tala Ksh 9 Milioni
Maafisa wa Idara ya Upelelezi (DCI) walimkamata raia kutoka Ghana anayeaminika kupokea KSh 9 Milioni kutoka kwa meneja wa mtandao wa kukopesha pesa.
Mshukiwa, Victor Anane atanchunguzwa kwa madai ya kumtapeli meneja wa kike kutoka Tala ambaye walikutana naye katika mtandao wa kuchumbiana.
4. Emmah Shisoka Ateuliwa Kuwa Katibu wa Chama cha Wasioamini Mungu Yupo
Chama cha wasioamini Mungu yupo kilimteuwa Emmah Shisoka kuwa katibu mpya baada ya Seth Mahiga kujiuzulu Jumamosi, Mei 29. R
Mahiga alidai amempata Mungu na kwa sasa anaamini yupo na pia yuko tayari kumtumikia.
5. Kanze Dena Afanya Kosa Wakati wa Kuhutubia Wanahabari Kisumu
Msemaji wa Ikulu alijipata pabaya baada ya kufanya kosa alipokuwa akihutubia wanahabari Jumamosi Mei 29 Kisumu.
Kanze alisema Rais wa Burundi Évariste Ndayishimiye atawasili nchini Jumatatu tarehe 'thelathini na tano'.
Msemaji huyo wa Ikulu alitaka kumaanisha Jumatatu tarehe thelethini na Moja Mei lakini ulimi wake ukateleza.
Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia news@tuko.co.ke au WhatsaApp: 0732482690.
Subscribe to watch new videosChanzo: TUKO.co.ke
ncG1vNJzZmijmajEorTIpaBnrKWgvG%2BvzmeinmdkZoFzgZBmopqmqpp6pbHNmmSam5ikuqatjKKirqSlYr2qr8eaZKeZXZ2uo63RomSzoZ6ctq%2BxjLOYZqOlqLa0tcyumGavmaC2brTIomWhrJ2h