Mtihani wa KCSE 2020: Wanafunzi Zaidi ya 280 Kukosa Matokeo

- Mtahiniwa Simiyu Robinson Wanjala wa Shule ya Upili ya Murang'a ndiye aliyeibuka mshindi kwa kupata maksi 87.334 - Watahiniwa wengine 893 walipata gredi ya A kwenye mtihani huo - Hata hivyo, Waziri Magoha ametangaza kwamba watahiniwa wengine 287 hawatapata matokeo yao kwa sababu walijihusisha na wizi wa mitihani

- Mtahiniwa Simiyu Robinson Wanjala wa Shule ya Upili ya Murang'a ndiye aliyeibuka mshindi kwa kupata maksi 87.334

- Watahiniwa wengine 893 walipata gredi ya A kwenye mtihani huo

- Hata hivyo, Waziri Magoha ametangaza kwamba watahiniwa wengine 287 hawatapata matokeo yao kwa sababu walijihusisha na wizi wa mitihani

Wizara ya Elimu imetangaza rasmi matokeo ya mtihani wa kitaifa wa kidato cha nne hii leo Jumanne, Mei 10 ambapo mwanafunzi bora alipata gredi ya A.

Habari Nyingine: Orodha ya Wanafunzi Waliofanya Vibaya katika Mtihani wa KCPE na Sasa Wameng'aa KCSE

Habari Nyingine: Nairobi Yashuhudia Mvua Kubwa Iiliyonyesha Usiku Kucha : "Tumeogelea si Kidogo"

Mtahiniwa Simiyu Robinson Wanjala wa Shule ya Upili ya Murang'a ndiye aliyeibuka wa kwanza kwa maksi 87.334.

Hata hivyo, Waziri George Magoha ametangaza kwamba watahiniwa 287 wa mtihani huo hawatapokea matokeo yao kwa ajili ya kujihusisha na udanganyifu wakati wa mtihani.

Magoha alisema wanafunzi hao walinaswa kwa kujaribu kuiba mitihani kwa kutumia simu za rununu au maandishi kwenye sare zao za shule.

Akihutubia taifa akiwa katika jumba la Mtihani House, Waziri Magoha alisema shule zote zitapokea matokeo ya mtihani huo japo huenda kukawa na mabadiliko baada ya kukamilika kwa uchunguzi unaoendelea.

Habari Nyingine: Matokeo ya KSCE 2020 yametangazwa, 893 wapata gredi ya A

Kulingana na arifa ya Magoha, shule 20 huenda zitakosa kupokea matokeo ya mtihani iwapo zitapatikana na hatia ya wizi wa mitihani.

Kama ilivyoripotiwa awali na TUKO.co.ke, watahiniwa 893 walipata gredi ya A huku 143, 140 wakipata alama zitakazowawezesha kuingia moja kwa moja katika Vyuo Vikuu.

Takwimu za Baraza la kitaifa la mitihani nchini, KNEC zinaonyesha kuwa watahiniwa 752,933 walisajiliwa kufanya mtihani wa KCSE mwaka uliopita katika vituo 10,437.

Mtahiniwa Simiyu Robinson Wanjala wa Shule ya Upili ya Murang'a ndiye aliyeibuka mshindi kwa kupata maksi 87.334 ikiwa ni gredi ya A.

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia news@tuko.co.ke au WhatsaApp: 0732482690.

Tazama habari zaidi kutoka TUKO.co.ke

Subscribe to watch new videos

Chanzo: TUKO.co.ke

ncG1vNJzZmijmajEorTIpaBnrKWgvG%2BvzmeinmdkZn52gpVmpK2hmJa7qnnWmmSkm6OaenN8kWlksJmelrO2utmiZLOZmZm2bsXAZmlxaF2gwqy70ppkppmkpLimu42hq6ak

 Share!