Magazeti Alhamisi, Machi 25: Ndoa ya NASA yaendelea Kuvunjika Vipande Huku Ikisambaratika

Magazeti ya Alhamisi Machi 25 yamezamia taarifa kuhusu mzozo unaoendelea ndani ya muungano wa NASA baada ya kutimuliwa kwa Seneta Cleophas Malala kutoka wadhifa wa naibu kiranja wa seneti. 1. Standard

Magazeti ya Alhamisi Machi 25 yamezamia taarifa kuhusu mzozo unaoendelea ndani ya muungano wa NASA baada ya kutimuliwa kwa Seneta Cleophas Malala kutoka wadhifa wa naibu kiranja wa seneti.

1. Standard

Taarifa kuu kwenye Standard ni kuhusiana na hatua ya maseneta wa ODM kumtimua Cleophas Malala kutoka naibu kiranja wa seneti.

Malala alikuwa amekabidhiwa wadhifa huo baada ya uchaguzi wa 2017 ambapo chama chake cha ANC kilikuwa kwenye uhusiano mzuri na ODM chini ya mwavuli wa NASA.

Hata hivyo, ni wazi sasa kuwa ndoa ya NASA imevunjika na watoto wameanza kupitia magumu kama vile kutimuliwa kutoka nyadhifa wanazoshikilia.

Hatua ya ODM kumtimua Malala ilikashifiwa vikali na kiongozi wa ANC Musalia Mudavadi na mwenzake wa Ford Kenya Moses Wetangula.

2. Nation

Taarifa kwenye Nation ni kuhusu chanjo inayoendelea dhidi ya janga la coronavirus huku wengi wa Wakenya wakisema wanahofia iwapo ni salama.

Viongozi mbali mbali wamekuwa wakimtaka Rais Uhuru Kenyatta kuongoza katika kuchanjwa ili Wakenya wawe na imani na dawa hiyo.

Aidha kuna taarifa pia kuhusu wakazi wa Homa Bay ambao wameishtaki kampuni ya Coca cola kwa kuharibu mti uliopandwa eneo hilo na kiongozi wa upinzani Raila Odinga.

Dereva wa kampuni hiyo aliharibu mti huo alipokuwa akirudi nyuma na wanaharakati watatu wakaelekea mahakamani.

Wamekuwa wakitaka kampuni hiyo ifadhili safari ya Raila eneo hilo ili kupanda mti mwingine.

3. Star

Gazeti la Star limeangazia siasa za chama kipywa kinachohusishwa na Naibu Rais William Ruto cha United Democratic Alliance.

Chama hicho kilizindua katiba yake ambayo inatoa nafasi kwa 'hustlers' kushikilia nyadhifa za uongozi.

Aidha, si lazima kiongozi wa chama hicho awe ndiye mgombea wa urais na hivyo kumaanisha kabwela yeyote anaweza kushika nafasi hiyo.

4. Taifa Leo

Mhariri wa Taifa Leo anatujuza kuwa kuna chanjo mpya dhidi ya Covid-19 imeingia na sasa wenye mapeni hawatasubiri ile inatolewa na serikali.

Hospitali za kibinafsi zimeleta chanjo hiyo na sasa wenye fedha watahitajika kulipa kati ya 8, 000 na 11, 000 kuipokea.

READ ENGLISH VERSION

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia news@tuko.co.ke au WhatsaApp: 0732482690.

Tazama habari kemkem za TUKO hapa

Subscribe to watch new videos

Chanzo: TUKO.co.ke

ncG1vNJzZmijmajEorTIpaBnrKWgvG%2BvzmeinmdkZYN5fpRmpJqfka%2BytbWMmqOhmZ2ewKp5zZ2mmmWplnqvrdKaZLKZlaOxprjEmmSkraOWuqOt0ZqroqORY7W1ucs%3D

 Share!