Magazeti ya Alhamisi, Juni 11: Raila avuna unono huku DP Ruto akibanwa na bajeti

Kuzinduliwa kwa bajeti ya 2020/2021 ambayo inatazamiwa kusomwa leo ndio taarifa yenye uzito kwenye magazeti ya Alhamisi, Juni 11. Kulingana na magazeti haya, kusomwa kwa bajeti mwaka huu kunafuatwa kwa karibu sana na wananchi huku ikikujia wakati taifa hili linakupambana na mafuriko, uvamizi wa nzige na janga la COVID-19 ambalo limeleta madhara kubwa.

Kuzinduliwa kwa bajeti ya 2020/2021 ambayo inatazamiwa kusomwa leo ndio taarifa yenye uzito kwenye magazeti ya Alhamisi, Juni 11.

Kulingana na magazeti haya, kusomwa kwa bajeti mwaka huu kunafuatwa kwa karibu sana na wananchi huku ikikujia wakati taifa hili linakupambana na mafuriko, uvamizi wa nzige na janga la COVID-19 ambalo limeleta madhara kubwa.

Habari Nyingine: Picha za mazishi ya George Floyd iliyihohudhuriwa na maelfu ya watu tajika

Habari Nyingine: Kocha Juanma Lillo achukua mikoba ya Mikel Arteta katika klabu ya Man City

1. People Daily

Katika hali ya kawaida, siku ya kusoma Bajeti ni siku ambayo kila Waziri wa Hazina ya Taifa hutamani iwe rahisi.

Hata hivyo, 2020 sio mwaka wa kawaida, Waziri wa Fedha Ukur Yatani atatabasamu endapo ataweza kwani atakuwa amevalia barakoa huku akifichua bajeti ya KSh 3.2 trilioni ambayo inatazamiwa kuweka Kenya dhabiti kwa mwaka mmoja huku ikipambana na COVID-19.

Kulingana na mizani, ili kuhakikisha kuwa masomo yanaendelea shuleni, Tume ya Kuwaajiri Walimu (TSC) inaondoka na donge kubwa ya KSh 266. 1 bilioni.

Wizara ya uchukuzi imetengewa KSh 189. 6 bilioni ambayo imepungua kwa KSh 50.6 bilioni tofauti na 2019/2020, Afya (KSh 117.6 bn), Usalama wa Ndani (KSh 131.7 bn) huku KSh KSh 33.6 bn zikiekezwa kwa usalama wa umma.

Hata hivyo, Wakenya wana wasiwasi ya namna Yatani ataweza kufadhili bajeti hiyo huku kukiwa na hali mbaya ya uchumi iliyochangiwa na idadi kubwa kupoteza ajira.

2. The Star

The Star linaripoti kuhusu madai ya serikali ya Burundi kuwa Rais anayeondoka Pierre Nkurunziza alifariki kutokana na mshtuko wa moyo.

Kulingana na gazeti hili, kiongozi huyo ambaye alikuwa anatazamiwa kumkabithi mamlaka rais aliyechaguliwa mnamo Agosti, alifariki kutokana na COVID-19, ugonjwa ambao alikuwa ameweka siri na hata kuwafurusha maafisa wanne wa WHO nchini humo.

Kabla ya kifo chake, madaktari walikuwa njia panda kuhusu kumsafirisha hadi Nairobi ama Dar es Salaam kwa matibabu lakini aliaga dunia kabla ya uamuzi kufanywa.

Mke wake ambaye alikuwa anaugua ugonjwa huo alirejea Burundi kutoka Hospitali ya Nairobi ambapo alikuwa anapokea matibabu.

3. Taifa Leo

Gazeti hili linaripoti kuwa Ofisi ya Naibu Rais William Ruto ndio imeathirika pakubwa katika kupunguziwa bajeti na Hazina ya Taifa huku ikipania kufadhili bajeti ya KSh 3.2 trilioni.

Ofisi ya Ruto imepungiziwa bajeti yake kwa KSh 988 bilioni kutoka kwa 2.4 bilioni hadi 1.4 bilioni katika mwaka wa kifedha wa 2020/2021 huku Ofisi ya Rais Uhuru Kenyatta ikiongezwa kutoka KSh 11.4 hadi KSh 36.6 bilioni.

Huku Ruto akijistiri na bajeti hiyo ndogo, kiongozi wa Upinzani Raila Odinga ana tabasamu huku ofisi yake ikitengewa KSh 71.9 milioni.

Raila pia anatazamiwa kunufaika kutoka kwa KSh 26 milioni ya kununua magari, bima (KSh 20 milioni) na KSh 10 milioni ya fanicha.

Miongoni mwa gharama iliyoondolewa katika ofisi ya Naibu Rais ni usafiri wa humu nchini ambayo imepunguzwa kutoka KSh 193 milioni hadi KSh 96 milioni huku gharama za usafiri za kigeni ikipunguzwa kutoka KSh 89 milioni hadi KSh 33 milioni.

Uwezo wa Ruto kuwaburudisha wageni pia ilibanwa kutoka KSh 187 milioni hadi KSh 87 milioni..

Gharama ya mafuta pia ilipunguzwa hadi KSh 14 milioni kutoka kwa KSh 28 milioni huku shughuli za kila siku zikitengewa KSh 103 milioni kutoka kwa KSh 307 milioni afisi hiyo ilipokea mwaka jana.

4. The Standard

Gazeti hili linachunguza sababu za viongozi wanaomuegemea Naibu Rais William Ruto wamekuwa wakikimbia katika ofisi ya Raila Odinga ya Capitol Hill.

Kulingana na The Standard, viongozi hao wamekuwa wakimtembelea Raila kuunga mkono maridhiano na ni njia ambayo Rais Uhuru Kenyatta anatumia kurejesha ungwaji mkono kutoka kwa viongozi wa Mlima Kenya.

Mgeni wa hivi majuzi Capitol Hill alikuwa Mbunge wa Laikipia Kaskazini, Sarah Korere ambaye anatambulika kwa kumtaja Raila kama mwanasiasa asiyekuwa na makali ambaye anatakiwa kuwapisha viongozi vijana kama William Ruto.

Gazeti hili linaripoti kuwa Uhuru Kenyatta kwa sasa ana wabunge wengi kutoka eneo hilo ambao wanamuegemea lakini wengine wameweka mizizi kwa Ruto.

5. Daily Nation

Spika wa Seneti Kenneth Lusaka amesema Bunge hilo litakutana hii leo Alhamisi, Juni 11, kubuni kamati ambayo itaanzisha mchakato wa kusikiza hoja ya kumbandua Gavana wa Kirinyaga, Anne Waiguru ambayo ilipitishwa na bunge la kaunti.

Kamati hiyo inaweza kuamua kubuni kikosi kitachochunguza suala hilo na kuwasilisha ripoti Seneti chini ya siku 10 kuhusu madai yaliyoibuliwa dhidi ya Waiguru na madiwani wa Kirinyaga.

Bunge hilo pia linaweza kuamua kujigeuza kuwa kamati, kutathmni suala hilo na kisha mwishowe kupiga kura ya kuamua hatma ya gavana huyo.

Waiguru,kwa mara ya tatu, amekimbia mahakamani kutafuta idhini ya kutupiliwa mbali kwa uamuzi wa mawakilishi wadi kwa kuandaa kikao hicho licha ya korti kusitisha kusikizwa kwa hoja hiyo.

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia news@tuko.co.ke au WhatsaApp: 0732482690.

Subscribe to watch new videos

Chanzo: TUKO.co.ke

ncG1vNJzZmijmajEorTIpaBnrKWgvG%2Bvzmeinmdja356hJBmpJqfka%2BytbWMsphmmZydrq610qJko62ennpyfYyrmKKkkWKut8HNmmSupp%2BjvG601KSsZpygYr%2B2wM5mmKShkpa7uK2Mp5hmmpGfsrW1jaGrpqQ%3D

 Share!