Raila alinituma kwa mganga 2017, mbunge asema

- Baraza alisema Raila alimtuma kwa mganga mmoja kutafuta nguvu za kishirikina - Mbunge huyo amedia ana ushahidi kuwa kiongozi huyo wa ODM hushiriki ushirikina kwenye siasa zake - Alisema alishangaa kuwa mbunge Simba Arati alifika Kibra na vijana waliomtimua

- Baraza alisema Raila alimtuma kwa mganga mmoja kutafuta nguvu za kishirikina

- Mbunge huyo amedia ana ushahidi kuwa kiongozi huyo wa ODM hushiriki ushirikina kwenye siasa zake

- Alisema alishangaa kuwa mbunge Simba Arati alifika Kibra na vijana waliomtimua

Mbunge wa Kimilili Didmus Barasa amedai kuwa Raila Odinga ni kiongozi ambaye huamini mbinu za kishirikina katika siasa zake.

Barasa alisema alishangazwa sana alipoenda kutafuta ushauri wa kisiasa kwa kiongozi huyo wa ODM na badala yake akamtuma Nigeria kwa mganga.

Habai Nyingine: Magazeti ya Kenya Ijumaa, Novemba 15: Mkutano wa Rais Kenyatta watingisha ulingo wa siasa

Kwenye mahojiano na mtangazaji wa TUKO.co.ke Kevin Philips, Barasa alisema alimtafuta Raila baada ya kutathmini hali na kuona chama chake cha Ford Kenya wakati huo hakingempa ushindi.

"Nikuwa ndani ya Ford Kenya na mpinzani wangu alikuwa ndiye mwelekezi wa uchaguzi chamani na pia mfadhili. Nikaona hapo sina nafasi bora na ndio nikatafuta ushauri wa Baba ambaye aliniahidi tiketi ya chama na pia tukajadili mambo mengi," alisema."Lakini alianza kucheza michezo na kuniambia niende nionane na mzee ambaye ni rafiki yake na kuniambia nisijali kuhusu pesa kwa sababu kuna njia nyingine. Kama mkatoliki, nikagundua kuwa napelekwa njia ya uganga na ndipo nikaachana naye," aliambia mwandishi wetu.

Habari Nyingine: Wasiwasi baada ya Rais Kenyatta kuita wabunge wake kwenye mkutano Nyeri

Alisema hilo lilimfanya kuachana na kusaka tiketi ya ODM na badala yake akaingia Jubilee ambapo aliishia kupata ushindi.

Mbunge huyo ambaye amekuwa kikemea Raila na kumuita mganga alisema ana ushahidi kuonyesha kuwa kiongozi huyo wa upinzani hutegemea nguvu za kishirikina kwa manufaa ya kisiasa.

Mbunge huyo aliendelea kumshtumu Raila na kudai yeye ni kiongozi laghai.

"He used to condemn Uhuru of presiding over a corrupt country, you would imagine the president was presiding over a casino. He has now changed the tune and is saying Uhuru is good but his deputy is bad. Those are signs of a man who has reached political menopause," he said.

"Aliishi kumkemea Uhuru akisema anaendesha serikali fisadi kiasi ungefikiria rais anendesha mchezo wa pata potea. Kwa sasa amebadili na kusema Uhuru ni mzuri na Ruto ni mbaya. Hiyo ni dalili za mtu aliyefika umri wa kustaafu kisiasa," alisema mbunge huyo.

Baraza alijipata pabaya wakati wa uchaguzi wa Kibra Novemba 7 baada ya kushambuliwa na kundi la vijana waliokuwa wameandamana na mbunge wa Dagoretti Kaskazini Simba Arati.

Alisema hatua hiyo ilimshangaza kwani wamekuwa marafiki na Arati tangu siku zao kama viongozi wa wanafunzi.

"Nilihudumu kama kiongozi wa wanafunzi katika chuo cha Kenya Power Training College na nilikuwa nakutana na Simba Arati ambaye alikuwa kiongozi katika chuo cha Kenya Polytechnic. Tulikuwa tukikutana na kujadili masuala kadhaa," alsiema.

READ ENGLISH VERSION

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia news@tuko.co.ke au WhatsApp: 0732482690.

Subscribe to watch new videos

Chanzo: TUKO.co.ke

ncG1vNJzZmijmajEorTIpaBnrKWgvG%2BvzmeinmdjZ4F4fpBmqZqhnJZ6orjIp6CtrZ2WeqzDwGakoJmenK5ufo9qbmalkqq7qLGMmqqepZFjtbW5yw%3D%3D

 Share!