- Millie amesema Jubilee wako huru kugombea ubunge Kibra
- Mbunge huyo alimkosoa Babu Owino kwa kukosoa Rais Kenyatta kwa kumuunga mkono Mariga
- Millie alisema mashindano ni lazima lakini Jubilee hawatapata lolote Kibra
Mbunge wa Suba Kaskazini Millie Odhiambo ameunga mkono hatua ya Rais Uhuru Kenyatta kupigia debe mgombea wa Jubilee kwenye uchaguzi mdogo wa Kibra McDonald Mariga.
Wakati uo huo , Odhiambo alimkosoa mbunge wa Embakasi Mashariki Babu Owino kwa kumkejeli rais kutokana na uamuzi wake wa kupigia debe Jubilee.
Habari Nyingine: Polisi wamulikwa kuhusiana na wizi katika kiwanda cha Humphrey Kariuki cha Thika
Akiongea kwenye mahojiano na Citizen TV, Jumatano Septemba 18, Odhiambo alisema mwafaka wa siasa kati ya Rais Uhuru Kenyatta na Raila Odinga haumaanishi kuwa hakutakuwa na mashindano.
"Owino na mimi tuko katika kiwango tofauti na pia tajriba tofauti. Yeye akiona handisheki, anafikiria Jubilee haifai kuwa na mgombea," alisema Odhiambo."Lakini sifikirii hivyo, lakini atajifunza kuwa mwafaka huo haumaanishi kuwa wapinzani wetu hawatashindana na sisi," aliongezaHabari Nyingine: Shabiki aikwamia suti ya Harmonize jukwaani wakati akimtumbuiza Rais Magufuli
"Baba lazima awe mwangalifu na hii handisheki. Hatujapata matunda yoyote na hatuwezi kupumbazwa mara mbili. Uhuru lazima awe mkweli na hii handisheki," alisema Babu OwinoMillie, hata hivyo, alisema wafuasi wa ODM hawafai kuwa na wasiwasi kwani eneo bunge la Kibra ni ngome ya ODM na lazima mgombea wake aibuke mshindi.
Aliongeza kuwa Mariga ni mradi wa Naibu Rais William Ruto ambapo anajaribu kuonyesha ubabe wake wa kisiasa katika mashindano na Raila Odinga.
"Kibra ni ODM na ODM ni Kibra," alisema OdhiamboREAD ENGLISH VERSION
Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia news@tuko.co.ke au WhatsApp: 0732482690.
Subscribe to watch new videosChanzo: TUKO.co.ke
ncG1vNJzZmijmajEorTIpaBnrKWgvG%2BvzmeinmdjZoJ5hI9mpKKknJ6ybrvDoaCapZKkeqLBzaCYZqWbpLuwedShrKutXaCutbXKmmSumZ2qx6p51ppkpKGSp65vtNOmow%3D%3D